; Sherehe ya kutangaza Vivutio Saba vya Asili Barani Afrika kufanyika jijini Arusha Tanzania tarehe 11 February 2013 » Tanzania Tourist Board
 
Language English Kiswahili

Sherehe ya kutangaza Vivutio Saba vya Asili Barani Afrika kufanyika jijini Arusha Tanzania tarehe 11 February 2013

By: Geofrey Tengeneza

Sherehe za kutangaza vivutio vya asili vya bara la Afrika zinategemea kufanyika katika hoteli ya Mt Meru katika jiji la Arusha Tanzania tarehe 11 February 2013 kuanzia saa nane mchana.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania viongozi mbali mbali wa kitaifa na kimataifa ambazo wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda. Rais wa Taasisi iliyoendesha shindano hilo la kutafuta Maajabu hayo Saba la Seven Natural Wonder Dr Philip Imler kutoka Marekani anatarajiwa kuwasili tarehe 9/2/2013 tayari kabisa kutangaza vivutio Saba vya Asili vya bara la Afrika.

Tanzania ilikuwa na vivutio vitatu vilivyoingia kwenye kinyanganyiro hicho ambavyo ni Mlima wa Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na wanyama wanaohama wa Seregeti. Tanzania imekwisha tajwa kuwa miongoni mwa washindi ambao angalau kivutio kimoja ama zaidi Saba ya Asili Afrika.

Macho na masikio ya watanzania ni kujua ni kivutio au vivutio gani hivyo vya Tanzania vimeweza kushinda.

 

 

 

Contact Information

Contacting us by post Tanzania Tourist Board
Utalii House - Laibon street/Ali Hassan Mwinyi Road - Opposite French Embassy
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email md@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General: +255 22 2664878/9
Marketing:+255 22 2664875
Tourism Services:+255 22 2664873
  • Branch Offices
  • Contacting us by fax

    Did you know!

    That Freddy Uiso, is the only contestant from Africa to participate in the World Chef Championship Competition and to be nominated for World Chef Title and become the 4th winner?".

    S!TE TO RESUME 2017!