; TTB YAENDELEA KUHAMASHISHA UTALII WA NDANI KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA YA DAR ES SALAAM » Tanzania Tourist Board
 
Language English Kiswahili

TTB YAENDELEA KUHAMASHISHA UTALII WA NDANI KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA YA DAR ES SALAAM

Idadi kubwa ya wananchi wanaopata fursa kutembelea banda la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) lililopo ndani ya jeno la Wizara ya Maliasili na Utalii wanaoneka kuhamasika zaidi na suala zima la Utalii wa ndani ambalo TTB inaonekana kulipa msukumo wa pekee kwa lengo la kuhakikisha watanzania wanahamasika kutembelea vivutio vilivyomo katika nchi yao na kuondokana na dhana kuwa vipo kwa ajili ya wageni tu kutoka nje ya nchi.

Hali hiyo imedhihirisha katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam ambapo wananchi wengi wamekuwa wakiulizia na kupata ufafanuzi zaidi kuhusu umuhimu wa wao kutembelea vivutio vyetu na suala zima la kukuza utalii wa ndani huku wengi wakionesha kuhamasika kutembelea vivutio hivyo.

William Halule (kushoto) na Elirehema Maturo(Kulia) wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakitoa maelezo kwa baadhi ya wageni waliotembelea banda la TTB lilioko katika jingo la wizara ya Maliasili na Utalii katika maonesho ya Kimataifa ya Dar es salaam.

Wananchi wengi ambao wamekuwa wakitembelea banda la Bodi ya Utalii wamekuwa wakidadisi zaidi kuhusu gharama za kutembelea vivutio mbalimbali na umuhimu wa utalii wa ndani katika kuinua uchumi wa nchi. Aidha wamekuwa wakihoji kuhusu vivutio vya Tanzania vilivyoshinda na kuingizwa katika orodha ya maajabu Saba ya Asili Barani Afrika ambavyo ni Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (kwa maana ya nyumbu wahamao) Kreta ya Ngorongoro, na Mlima Kilimanjrao.

Pamoja na kushiriki katika jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii lilioko katika viwanja hivyo vya maonesho,  Bodi ya Utalii Tanzania inashiriki pia katika banda la PTA sambasamba na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro (NCAA). Banda la PTA mwaka huu ni mahsusi zaidi kwa makampuni na waoneshaji kutoka nje ya nchi.

Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 28/06/2013 na kushirikisha waoneshaji kutoka ndani na nje ya nchi yanatarijiwa kuhitimishwa tarehe 8/7/2013.

Contact Information

Contacting us by post Tanzania Tourist Board
Utalii House - Laibon street/Ali Hassan Mwinyi Road - Near French Embassy
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General: +255 22 2664878/9
Marketing:+255 22 2664875
Tourism Services:+255 22 2664873
Mobile:+255 737229549
 • Branch Offices
 • Contacting us by fax

  Did you know!

  That "the name Selous game reserve originates from Captain F.C Selous, an English man lived in the area some many years back who was killed by Germans in the First World War and buried in the same area?

  S!TE 2016!

  nero free download
  daemon tools free download
  roxio creator free download
  download angry birds for pc free
  adobe master collection cs5 serial
  wpe pro free download
  microsoft office 2007 free download