; NISHANI ZA UTALII » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

NISHANI ZA UTALII

Utaratibu wa kutoa Nishani za Utalii ulitangazwa rasmi na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwenye Mkutatano wa ATA uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia mwezi Mei, 2000. Nishani hizi, ambazo ni za kila mwaka, zilitolewa kwa mara ya kwanza Jijini Cape Town, Afrika ya Kusini kwenye Tamasha la Chakula cha Jioni la Mkutano wa ATA uliofanyika Mei, 2001.

Madhumuni ya Nishani hizi, ambazo siku zote hutolea na Waziri wa Maliasli na Utamaduni, ni kuwatunuku waendeshaji wa biashara ya usafiri wa kitalii na waandishi wa habari mahiri kwa mchango wao wa kuiuza Tanzania, hususani kwenye soko la Marekani, na kutambua mchango wa ATA wa kukuza Utalii wa Bara la Afrika.  Moja kati ya maeneo ambayo TTB imekusudia kutangaza ni ukanda wa Kusini wenye vivutio vilivyokuwa havijulikani kwenye soko la Utalii.

Mwaka 2004 TTB ilibuni Nishani ya Kiutu inayotolewa kwa makampuni ya biashara ya kutembeza wageni. Hii ilitokana na Mkutano Mkuu wa Pili wa Amani kupitia Utalii Barani Afrika (IIPT) ulioandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Jijini Dar es Salaam, Desemba, 2003. Nia hasa ya TTB ilikuwa ni kuwahamasisha wanaoendesha biashara hii kuchangia na kuboresha maisha ya jamii na kuwafanya nao wawe wadau katika sekta ya utalii.

Katika mwaka huo huo  wa 2004, TTB ilipanua wigo wa Mpango huu ili kuwatunuku pia wadau wazalendo ambao kwa njia moja au nyingine katika uboreshaji  wa miundombinu za Utalii nchini, kwani bila mchango wao kiwango hiki cha ukuaji kisingefikiwa.

Wakati TTB ikisherehekea mwaka wake wa 11 wa mafanikio ya Utoaji wa Nishani za Utalii,  sekta imekua kwa kiwango kuridhisha, hasa ikitiliwa maanani Taifa linasherehekea Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.  Katika sherehe hizi Mpango huu utaelekezwa kwenge anga la kimataifa.

Orodha ya Nishani hizi tangu 2001 hadi 2011 zinapatikana hapa.

 

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?