SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA
Karibu tusherehekee pamoja Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara! Angalia Ratiba ya Sherehe ! Tumethubutu, Tumeshinda, Tunasonga mbele!
RATIBA
The Kilimanjaro Uhuru Climb, Moshi Desemba 4 – 7, 2011
Watu 200 kutoka sehemu mbali mbali duniani watashiriki Matembezi Makubwa ya Kupanda Mlima Kilimanjaro yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) na Kampuni ya Kutembeza Watalii ya Zara ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Washiriki watatumia njia nne tofauti na kukutana “Kilele cha Uhuru” kwenye mkesha.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:
Zara Tanzania Adventures.
Simu No.+255 – 754-451000
E-mail: bookings@zaratours.com
Website: www.zaratours.com
Kili Festival, Dar es Salaam Desemba 7 – 11, 2011
Kili Festival, maarufu kama Kilifest, ni tamasha litakalojumisha maonyesho ya muziki aina mbali mbali, ngoma za kitamaduni na vyakula vya asili. Limeandaliwa na Clouds Entertainments ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na wafadhili mbali mbali.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:
Clouds Entertainments
Simu No. +255 – 22-27-81-44-5
Website: www.kilifest.com.tz
Nyerere Day Relay Marathon, Mwanza December 4, 2011
Mbio hizi za kupokezana za umbali wa kilometa 192 zitaanzia Mwanza mjini na kuishia kijiji cha Butiama, alikozaliwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mbio zitashirikisha wanariadha 100 watakaogawanywa katika vikundi 10, kila kimoja kikikimbia kilometa 19. Waandaaji ni Capital Plus ya Dar es Salaam.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:
Capital Plus International Ltd
Simu No. +255 – 713-388 758
Website: www.capitalplus.com.tz
Kilele cha Sherehe za Kumbukumbu ya Uhuru ni Desemba 9, 2011 katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.



Je ulikuwa wajua?


