; Hifadhi za Taifa » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Hifadhi za Taifa

Maelezo kuhusu vivutio vya Hifadhi za Taifa na Mbuga za Wanyama

Tanzania ni nchi pekee duniani iliyotenga eneo kubwa la ardhi yake kwa ajili ya hifadhi ya wanyamapori. Vivutio vingi, kuanzia miamba ya matumbawe ya kale, mbuga za wanyama pamoja na hifadhi za taifa na hata mabonde yaliyoko kwenye nyanda za juu, vyote vinalindwa na sheria ya nchi kwa ajili ya urithi wa vizazi vijavyo.

Pamoja na vivutio vingi vilivyopo nchini Tanzania, tumeongeza hifadhi nyingine ambazo umaarufu wake unafunikwa na zile zenye majina makubwa kama Serengeti na Ngorongoro. Kwa kuongeza vivutio hivi kwenye orodha yetu tunatumaini kwamba watalii wataweza kuviingiza katika ratiba ya safari zao na hatimaye kusaidia kuvitangaza.Vitalu vingi vya uwindaji hatukuvitaja kwa sababu ya kanuni na taratibu haziruhu watalii kuingia katika maeneo haya.

Tanzania ina bioanuwai ya kusisimua na sababu hiyo idadi ya wanyamapori na aina za ndege hutofautiana kulingana na msimu maeneo wanamoishi. Kwa hiyo ni jambo la busara pia kutembelea mojawapo ya mbuga ndogo ndogo za wanyama.

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?