Kuhusu TTB
KUHUSU BODI YA UTALII (TTB)
1.0 Utangulizi
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ni asasi ya kiserikali, iliundwa rasmi na Sheria ya Bodi ya Utalii Tanzania CAP 364 ya 1962 na kurekebishwa na Sheria Na.18 ya 1992. TTB ilianzishwa baada ya kuvunjwa kwa Shirika la Utalii Tanzania (TTC). Bodi imepewa mamlaka ya kukuza na kuendeleza shughuli zote za kitalii nchini Tanzania.
2.0 Dira
Kuhakikisha Utalii unaongoza katika kukuza pato la Taifa (GDP) ifikapo mwaka 2025.
3.0 Dhima
Kuhakikisha kuwa kuna Utalii endelevu wa ndani na nje kwa kutumia njia zote za ubunifu ili kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na uchumi.
4.0 Kazi za TTB
- Shughuli maalum za TTB ni kuchukua hatua zote inazoziona ni muafaka katika kuitangaza Tanzania kama nchi inayoongoza katika vivutio vya Utalii.
- Kuchukua hatua zote za maendeleo yenye mvuto kwa watalii kutembelea Tanzania.
- Kufanya utafiti wa kina na kuandaa mikakati ya mama ya kuboresha shughuli za Utalii.
- Kujenga uelewa ndani ya jamii kuhusu umuhimu na manufaa ya kiuchumi inayotokana na shughuli ya sekta ya Utalii.
- Kutafuta habari muhimu ambazo zitaleta tija kwenye utendaji katika shughuli za Bodi ya Utalii.
5.0 Bodi ya Wakurugenzi
TTB inayo Bodi ya Wakurugenzi ambayo huchaguliwa kila baada ya miaka mitatu. Mwenyekiti huteuliwa na Rais wa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania, ambapo Wajumbe wa Bodi huteuliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii.



Je ulikuwa wajua?


