; Bonde La Ngorongoro » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Bonde La Ngorongoro

Maelezo kuhusu vivutio vya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro

Bonde la Ngorongoro mara nyingi linajulikana kama ni “Eden ya Afrika” na linashika nafasi ya nane katika Maajabu ya Dunia. Kutembelea Bonde hili pia ni kivutio kikuu kwa watalii wanaopata fursa ya kuja Tanzania. Ndani ya Bonde kuna makundi makubwa ya punda milia na nyumbu ambao wakati mwingine hula majani karibu sana na simba wanaojipumzisha juani.

Alfajiri, faru weusi, ambao wako hatarini kutoweka, huenda kujificha kwenye misitu minene kufuata majani yaliyofunikwa na ukungu. Nje kidogo ya Bonde utakuta vijana wa Kimasai wanachunga mifugo yao wakichanganyika na wanyamapori, kitu ambacho wamekizoea kwa miaka mingi.

Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro linajumuisha bonde lenyewe maarufu, Korongo la Olduvai na maeneo makubwa ya uwanda tambarare na vichaka pamoja na misitu yenye ukubwa wa karibu kilometa za mraba 8300. Eneo hili limehifadhiwa na ni wenyeji tu ndio wanaruhusiwa kuishi karibu na huko.

Ndutu na Masek, ambayo ni maziwa ya chumvi ya magadi, pamoja na mfululizo wa vilima na volkano zake hufanya Eneo hili la Hifadhi kuwa makao makuu ya wanyama na ndege, hususan flamingo, maarufu na kivutio cha kipekee kwa watalii. Bonde lenyewe ambalo lina aina ya volcano inayojulikana kama ”caldera” ni kivutio kikubwa.

Sehemu za kulala wageni ziko kwenye ukingo. Unapotelemka unapitia mandhari ya misitu inayopungua unene mpaka unafikia bondeni. Ukiwa huko, utulivu wa wanyama unaowakuta ni wa kustaajabisha na unaweza kusahau kama uko kati ya wanayama hatari.

Mahali hapa pa ajabu ni makazi ya Korongo la Olduvai na ndipo familia ya Leakey walipogundua masalia ya binadamu yenye umri wa miaka milioni 1.8. Katika pango dogo linalotoa maji kaskazini mwa Bonde familia ya Leakey na kundi lake la wataalamu wa akiolojia walifanikiwa kufukua masalia ya viumbe vyenye asili ya mwanadamu inayokadiriwa kuwa na miaka milioni 3.7.  Huu ni uthibitisho kuwa hili ni  moja ya maeneo walipoishi binadamu wa mwanzo kabisa.

Bonde la Ngorongoro pamoja na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa kweli ni maeneo ya kuvutia sana hapa Tanzania hasa ukiunganisha mambo ya kihistoria pamoja na wingi wa wanyamapori. Ukiachilia mbali usafiri kwa magari kutelemkia bondeni na Korongo la Olduvai pamoja na vivutio vingine, bado misafara ya ketembelea Eneo zima la Hifadhi ya Ngorongoro inazidi kupata umaarufu.

 

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?