Gombe
Maelezo kuhusu vivutio katika Hifadhi ya Gombe
Hifadhi ya Taifa ya Gombe iko magharibi mwa Tanzania mpakani kabisa na Congo (DRC). Sifa zake zinatokana na Dk Jane Goodall, mwana sayansi na mtaalamu aliyetumia miaka mingi msituni akijifunza na kutafiti juu ya maisha ya sokwe-mtu, mnyama, ambaye sasa hivi yumo katika hatari ya kutoweka.
Gombe iko katika fukwe za Ziwa Tanganyika ikifunikwa na msitu mnene na ina mandhari nzuri ya Ziwa. Matembezi ya msituni na kuogelea ziwani ni baadhi ya viburudisho baada ya kutembelea “familia” ya sokwe-mtu.
Kweli kivutio mahsusi ni kutembelea maeneo zinamoishi “familia” za sokwe-mtu, ambapo unaweza kukaa na wanyama hawa wa ajabu kwa muda mrefu, jambo linalowavutia wageni wengi wanaotembelea sehemu hii ya Afrika. Licha ya sokwe-mtu, wanyama wengine maarufu wanaoishi katika misitu ya Gombe ni pamoja na kima, mbega, nguruwe pori, swala na aina mbali mbali ya ndege.



Je ulikuwa wajua?


