; Katavi » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Katavi

Pori la Hifadhi ya Taifa ya Katavi lililoko magharibi mwa Tanzania, ni kati ya maeneo ambayo hayajatembelewa na watu wengi. Hifadhi hii ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nchini, linatoa fursa ya kuona wanyama katika mazingira asilia. Katika Bara la Afrika, Katavi ni aina ya pekee ya hifadhi kwa upande wa wanyawapori, mimea na mazingira kwa ujumla.

Mabwawa yenye matete yaliyotapakaa hapa na pale ndiyo yanayoifanya Katavi kuwa makazi makuu ya viboko na aina mbali mbali ya ndege. Misitu ya upande wa magharibi ni hifadhi kubwa ya tembo na nyati. Maziwa ya msimu mara nyingi huwa na maji yaliyochafuka hasa kutokana na mvua zinaponyesha na pia wanyama wanapovamia kunywa maji. Hifadhi hii pia ni makazi maalum ya wanyama aina ya swala wenye rangi mchanganyiko na pia twiga weupe. Ni muhimu kutembelea ili kujionea maajabu ya Bara la Afrika.

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?