Mahale
Maelezo kuhusu vivutio vya Milima ya Mahale
Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale iko magharibi mwa Tanzania kando kando ya Ziwa Tanganyika kwenye mpaka wa Tanzania na Congo (DRC). Inafikika kwa usafiri wa ndege ndogo au boti. Ndani ya Hifadhi hii wanaishi sokwe-mtu wengi zaidi, ambao idadi yao inapita ile ya Hifadhi ya Gombe. Wanyama hawa wamezoeana sana na binadamu na hivyo ni rahisi makundi yao kuonekana.
Yeyote anayewaangalia kwa makini sokwe-mtu anaweza kutambua kuwabaadhi ya vitendo vyao vinakaribiana na vya wanadamu. Ukiachia mbali sehemu ambako milima hii ipo, safari ya kutembelea hawa wanyama ina manufaa makubwa na kwa mtu mwenye afya ya kawaida, mwendo wa kuwafikia walipo hauchoshi. Sokwe-mtu ni kati ya wanyama ambao sasa wako hatarini kutoweka.



Je ulikuwa wajua?


