; Mikumi » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Mikumi

Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iko Mkoani Morogoro kati ya Milima ya Uluguru na safu ya Lumango. Hifadhi hii ni ya nne kwa ukubwa nchini Tanzania na ni karibu sana kutoka Dar es Salaam katika barabara kuu iendayo Mbeya kupitia Iringa.

Watalii wengi wanaotembelea Hifadhi ya Mikumi wanapenda kuona wanyama maarufu “The Big Five”. Wanyama hao ni Chui, Simba, Faru, Tembo na Nyati. Idadi kubwa ya “mabwawa boko” huwawezesha watalii kuwasogelea karibu zaidi viboko ambao hupenda sana kucheza kwenye tope.

Kwa kuwa Hifadhi ya Mikumi iko karibu sana na Jiji la Dar es Salaam wageni wengi na baadhi ya wafanyabiashara hupendelea kwenda huko kwa mapumziko mafupi hasa wale ambao hawana muda wa kwenda mbali kwa shughuli za kitalii.

Mikumi inapakana na Milima ya Udzungwa pamoja na Mbuga ya Wanyama ya Selous na kwa pamoja hutengeneza ukanda maalum wa utalii.

 

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?