; Mkomazi » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Mkomazi

Hifadhi ya Mkomazi iko mashariki mwa Milima Pare ambayo ni sehemu ya ukanda wa Tao ya Mashariki na vile vile inapakana na nchi ya Kenya kwa upande wa kaskazini. Mahali hapa ndiko kunakoendeshwa mpango maalum wa kuwawezesha vifaru weusi, ambao wako katika hatari ya kutoweka, kuzaliana. Aina ya nyasi na mimeo katika eneo hili huwafaa sana faru.

Mkomazi sasa inaendelea kupata umaarufu hasa baada ya kupandishwa hadhi kutoka kwenye Mbuga ya Wanyama na kuwa Hifadhi ya Taifa. Ikilinganishwa na hifadhi nyingine nchini Hifadhi hii inasifika sana kwa kuwa na idadi kubwa ya mbwa-mwitu na kutokana na hali yake ya ukame wa mara kwa mara na kuwa na mawe mawe, nyoka wa aina pekee hupatikana kwa wingi sehemu hii.

 

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?