; Saadani » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Saadani

Saadani, ambayo hivi karibuni imepandishwa hadhi na kuwa Hifadhi ya Taifa, ni kiunganisho kizuri kati ya ufukwe wa bahari na nchi kavu na iko kilometa 70 tu kaskazini mwa mji wa Bagamoyo. Sehemu hii inafikika kwa urahisi kwa barabara toka Dar es Salaam na inatembelewa sana na watalii hasa wale wanaopenda kujipumzisha katika fukwe za bahari kati ya Dar es Salaam na Tanga.

Mto Wami ambao unapita kati kati ya Hifadhi ya Saadani na kumwaga maji yake katika Bahari ya Hindi ni makazi mazuri ya viboko, mamba, flamingo na aina nyingi ya ndege  wakubwa. Makundi ya tembo wanaonekana  wakiranda randa ufukweni karibu sana mto hasa majira asubuhi. Kitu cha pekee cha kuvutia katika Hifadhi ya Saadani ni kuona tembo wakifurahia kucheza na kasa katika povu la mawimbi  ya bahari.

 

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?