Udzungwa
Milima ya Udzungwa iko mkoani Morogoro na inaanzia mpakani mwa magharibi ya Mbuga ya Wanyama ya Selous. Tumbili na mbega wanatamba kwenye misitu minene, ambapo swala na wanyama wengine wadogo wadogo wanaonekana zaidi maeneo yasiyokuwa miti mingi. Hifadhi hii ina aina nyingi ya mimea inayovutia sana wataalam na ndege adimu ambao sasa wako kwenye hatari ya kutoweka.
Ingawa hakuna barabara katika milima hii lakini kuna njia tano mahsusi zinazowawezesha watalii na hasa wataalam waendao kwa miguu kujionea umaarufu wa hifadhi hii.Ukiwa kileleni unapata mandhari nzuri ya Mbuga ya Selous pamoja na kuiona pwani ya Bahari ya Hindi.



Je ulikuwa wajua?


