Arusha
Jiji la Arusha, maarufu kama “Mji Mkuu wa Utalii wa Tanzania” uko katika nyanda za juu kaskazini mwa nchi chini ya vilele “pacha” vya milima ya Meru na Kilimanjaro. Watalii wote wanaoelekea kwenye ukanda wa Utalii wa kaskazini huandaa safari zao Jijini Arusha linalojulikana pia kama “Geneva ya Afrika”.
Ukiwa kwenye mitaa ya Jiji la Arusha kilele cha Mlima Meru kinaonekana kama “Mlinzi wa Kifalme”, bonde lake limefunikwa na mawingu mazito huku mitelemko yake ikiwa na misitu minene. Kuwepo kwake karibu na hifadhi muhimu za Taifa, Jiji la Arusha ni mahali muafaka pa kupumzika kabla ya kuanza inayosubiriwa kwa hamu kubwa.
Kihistoria, mji wa Arusha ulianza kutambulika mwanzoni mwa karne ya 20 ukiwa kama kituo kidogo cha ulinzi wakati wa utawala wa ukoloni wa Wajerumani. Kituo hiki kilijengwa mahali panapofahamika kama Old Boma na kilikuwa kimezungukwa na bustani pamoja na maduka machache. Sasa hivi mji huu umepata hadhi kubwa kati ya miji maarufu nchini.
Umaarufu huo pia unauongezea mji wa Arusha kwa kuwa na makao ya Mahakama ya Kimataifa yanayoshughulikia Makosa ya Kimbari ya Rwanda na hapo ndipo yalipo Makao Mkuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na ni kitovu cha diplomasia na ushirikiano wa kimataifa, sifa zinazoufanya jiji hili kujulikana kama “Geneva ya Afrika”.



Je ulikuwa wajua?


