Bagamoyo
Mji wa Bagamoyo ulikuwa moja kati ya bandari maarufu katika pwani ya Afrika Mashariki kwa biashara na ni kituo cha mwisho cha misafara ya watumwa na meno ya tembo iliyosafirishwa kwa miguu toka Ziwa Tanganyika na hatimaye kuvushwa hadi Zanzibar. Katika harakati za kutokomeza biashara ya utumwa, Wamisionari waliufanya mji wa Bagamoyo, ambao kwa Kiswahili sahihi ulimaanisha “kubwaga moyo”, kuwa kitovu cha mikakati yao.
Siku hizi mji huu ni kituo kikuu cha kutengeneza majahazi katika pwani ya Tanzania. Mpaka sasa Bagamoyo ni mji tulivu ukiwa bado umepambwa na vivutio vya majengo ya kikoloni ya Wajerumani.



Je ulikuwa wajua?


