; Dar es salaam » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Dar es salaam

Mji la Dar es Salaam ulioko pwani ya Bahari ya Hindi ni mkubwa kuliko miji yote nchini na ni kitovu kikuu cha shughuli za kiuchumi. Jiji hili limekua sana hadi kufikia hadhi ya kuwa kiungo muhimu cha kiuchumi kati ya ukanda ya Afrika Mashariki na nchi nyingine. Hii ni bandari kuu nchini Tanzania.

Dar es Salaam ina viwanda vingi ambavyo huzalisha bidhaa  zinazotumika hapa nchini na bandari yake ni njia kuu ya kupitishia mazao mbali mbali yanayoingia nchini na kwenda nchi za nje. Ofisi kuu za Serikali, Ubalozi na mashirika mbali mbali ya umma na binafsi zina makao yao makuu Jijini Dar es Salaam.

Wakati wa himaya ya Mjerumani mwanzoni mwa karne ya 20, Dar es Salaam ilikuwa ndiyo makao yao makuu na ilikuwa ni kiungo muhimu kati ya bara na pwani pamoja na wafanyabiashara waliokuwa wakitumia Bahari ya Hindi. Vielelezo sahihi vya ukoloni wa Mjerumani na Mwingereza hasa usanifu wa majengo bado vinaonekana katika sehemu kadhaa za Jiji.

Wageni wanashauriwa kutembelea maeneo yenye vivutio vingi kama  Jumba la Makumbusho ya Taifa, Kijiji cha Makumbusho na masoko yaliyosheni vitu mbali mbali. Vivutio vingine vya kihistoria ni pamoja na Kanisa Kuu la Mt. Joseph na Jumba la Hatman karibu yake, Bustani ya Jiji, Ikulu na mandhari ya bahari na katikati ya Jiji.

Umbali wa kilometa saba kaskazini mwa Jiji kuna Hifadhi ya Kisiwa cha Bongoyo ambacho kinatoa fursa kwa wapenda michezo ya kuogelea na kupiga mbizi. Kisiwa kina ufukwe wa kuvutia na kimezungukwa na visiwa vidogo vidogo pamoja na aina nyingi ya viumbe wa bahari. Ingawa Hifadhi hii haina aina nyingi ya matumbawe na samaki kama ilivyo Unguja, Pemba na Mafia, bado inafaa kumpa mgeni nafasi ya kupumzika na kuangalia mandhari ya pwani ya Dar es Salaam.

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?