Dodoma
Mji wa Dodoma uko kati kati ya nchi na ndio Mji Mkuu wa Tanzania. Eneo la mji huu ni dogo na hauna maendeleo sana kulingalinisha na Jiji la Dar es Salaam. Ukiwa mashariki mwa nyanda za juu kusini, mji huu umezungukwa na mandhari nzuri na yenye ardhi inayofaa kwa kilimo na ufugaji na ni maarufu kwa kilimo cha zabibu na utengenezaji wa mvinyo.
Kihistoria, Dodoma ilikuwa sehemu kuu ya mapumziko kwa misafara iliyokuwa inatoka pwani kuelekea Ziwa Tanganyika. Serikali imeamua kuufanya mji wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya Bunge la Tanzania. Halikadhalika, Chama cha Mapinduzi kimeweka Makao yake Makuu huko huko.



Je ulikuwa wajua?


