Kigoma
Mji wa Kigoma uko kando kando mwa Ziwa Tanganyika ni mwanzo wa Reli ya Kati iliyojengwa na Mjerumani kuelekea Dar es Salaam. Mji huu ni makao makuu ya Mkoa na umezungukwa na milima na misitu ambayo inauletea mandhari nzuri, pia ni kiungo muhimu kibiashara na usafirishaji kati ya Tanzania na nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokerasia ya Congo, Rwanda na Zambia.
Kihistoria, Kigoma iko karibu na sehemu maarufu ya Ujiji ambako “wavumbuzi” Dk. David Livingstone na Henry Stanley walikutana kwa mara ya kwanza, pia kuna Nyumba ya Makumbusho ya maisha ya Dk Livingstone. Mji huu ni mwanzo wa safari za kitalii na kitaalam za kuelekea kwenye Hifadhi za Taifa za Gombe na Mahale.



Je ulikuwa wajua?


