; Kilwa » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Kilwa

Kilwa ina historia ndefu. Jina lenyewe lina asili ya Kireno, “Quiola”, kutokana na wafanyabiashara wa Kireno waliokuwa wanazunguka pwani ya mashariki ya Afrika katika Bahari ya Hindi.

Umaarufu wa Kilwa unarudi nyuma kwenye nyakati za Sindbad na hadithi zake za “Alfulela u Lela” na mtunzi wa mashairi wa Kireno, Milton, katika kitabu chake cha “Kilwa, Paradiso Iliyopetea”. Sifa nyingine ni kwamba Kilwa ilikuwa inajulikana kama “nchi ya Sultan Ali bin Hussain” aliyefahamika na wenyeji kama “Nguo Nyingi”. Hapa pia palikuwa ni njia kuu ya kupitishia biashara ya dhahabu kutoka iliyokuja kujulikana baadaye kama Rhodesia ya Kusini (sasa Zimbabwe) na kupitia Sofala (Msumbiji).

Vivutio vya Kilwa vinaweza kugawanywa katika sehemu nne (4). Mosi, Kilwa Kisiwani, ambayo iko kiasi cha kilometa mbili kutoka ufukwe wa bahari. Hapa ni uwanja waa mchanganyiko wa kiutamaduni baina ya wenyeji, Waarabu, Wareno, Wajerumani na baadaye Waingereza.

Majengo muhimu ambayo sasa ni magofu, ni pamoja na “Gereza” lililojengwa na Wareno na kukarabatiwa na Waarabu na kuligeuza kuwa “Ngome” yao. Kuna Msikiti Mkuu, Msikiti Mdogo, Kasri ya Sultani, kaburi la Sultani pamoja na makaburi ya maliwali 40 waliokufa katika ugomvi wa wenyewe kwa wenyewe.

Pili, Kilwa Kivinje, ambako watawala wa Kijerumani wakafanya ni Makao Makuu ya Serikali yao. Jengo la Boma hadi miaka ya hivi karibuni lilikuwa linatumika kama Mahakama na bado linadumisha historia ya sehemu hii mpaka leo.

Tatu, Kilwa Masoko, kama jina linavyojieleza ni sehemu ya biashara. Hapa Serikali ya kikoloni ya Mwingereza ilipafanya Makao Makuu ya Utawala na mpaka sasa Serikali ya Tanzania ina Makao ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Kivutio cha nne ni Kilwa Kipatimu, ndani kidogo kutoka ufukwe wa bahari. Wamisionari walifika Kilwa kujaribu kueneza dini ya Ukristo lakini walishindwa kumudu mazingira ya huko na walikimbilia Songea. Baadaye walirudi tena Kilwa lakini wakaamua kufanya makao yao Kipatimu ambako leo Ukristu umeshamiri sana.

Kilwa ni mashughuri kwa kuwa na fukwe zenye matumbawe muafaka kwa makazi salama ya kasa wa baharini na mazalia ya samaki. Kutegemeana na msimu viumbe wakubwa kama pomboo  na nyangumi, hutembelea sana sehemu hii. Jitihada zinaendelea kurudishia tena mikoko ambayo siku za nyuma ilisheheni sana ukanda huu. Kwa watalii wanaopenda michezo ya baharini hapa watapata burudani tosha.

 

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?