Mbeya
Jiji la Mbeya ni kati ya vituo maalum kwenye ukanda maarufu kwa kilimo katika nyanda za juu kusini-magharibi mwa Tanzania. Jiji hili ambalo ni makao makuu ya Mkoa wa Mbeya unaopakana na Zambia, liko kati ya milima ya Mbeya kwa upande wa kaskazini na milima ya Uporoto upande wa kusini-mashariki.
Mkoa wa Mbeya unajulikana sana kwa kuzalisha kahawa, chai, ndizi na kakao, mazao ambayo hupelekwa Mbeya mjini kwa ajili ya kusafirisha nje ya mkoa. Mazao mengine muhimu ya kilimo ni pamoja na mpunga, mahindi na viazi mviringo. Jiji la Mbeya ni makutano ya usafiri wa barabara na reli kwenda Malawi na Zambia.
Licha ya mafanikio katika kilimo kimkoa, mji wa Mbeya ulianzishwa rasmi kwenye miaka ya 1930 baada ya kugundulika madini ya dhahabu na kuwavutia wakazi na wawekezaji wengi. Ingawa dhahabu imepungua lakini bado inauletea mkoa mapato. Sasa hivi mkoa unajivunia kwa madini ya mkaa wa mawe huko Kiwira



Je ulikuwa wajua?


