; Mikindani » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Mikindani

Mikindani ni mji wa kihistoria kando kando mwa Bahari ya Hindi, karibu na bandari ya  Mtwara. Kuna pia uwanja mdogo wa ndege. Mandhari ya Mikindani inampa mgeni fursa ya pekee ya kujionea magofu ya kihistoria yanayohusu utamaduni wa watu pwani. Fukwe zake ni za kuvutia ingawa watalii wachache wamepata bahati ya kuzitembelea.

 

Kiutalii, sifa za mji wa Mikindani pamoja na Hifadhi ya Bahari ya Mnazi Bay na Mkondo wa Mto Ruvuma zinazidi vivutio kama hivi vilivyoko pwani yote kuelekea kaskazini.

Ukiwa mjini na kutembelea iliyokuwa ngome ya Mjerumani pamoja na soko la watumwa unakuta vivutio vingi pamoja na minazi iliyofunika fukwe hadi mpakani na Msumbiji.

 

Ukitumia boti kuelekea mkondo wa Mto Ruvuma unapata fursa ya pekee ya kutembelea hifadhi ya bahari yenye miamba ya matumbawe na viumbe wengine wa majini ambao hawajapata kuonwa na watalii wengi katika pwani hii ya Bahari ya Hindi.

 

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?