Morogoro
Morogoro ni kati ya maeneo muhimu katika sekta ya kilimo na mjini kuna viwanda vya tumbaku, ngozi, maturubai na mazulia kabla ya mazao hayo kusambaza kwenye masoko mengine. Pamoja na umaarufu katika kilimo, mji huu unafahamika sana kwa kupokea wamisionari wengi na matokeo ni kwamba hapa kuna idadi kubwa ya shule na hospitali za misheni.
Mji huu wa Morogoro uko chini ya Milima ya Uluguru na ni sehemu ya Milima ya Tao ya Mashariki. Watalii wengi wanaopenda kujiburudisha kwa matembezi ya kupanda milima ya Uluguru huanzia safari zao hapa mjini.
Milima hii inasifika kwa kuwa na misitu ambayo ni muhimu kwa vianzo vya maji na wataalam wa mimea wanakadiria kuwa misitu hii inaweza kuwa na umri wa miaka ipatayo milioni 25. Kwenye misitu kuna aina nyingi za ndege na wadudu.



Je ulikuwa wajua?


