Moshi
Mji wa Moshi uko chini ya Mlima Kilimanjaro ambao ni mashuhuri na mrefu kuliko yote barani Afrika, na ni kivutio kikubwa cha kimataifa kwa watalii. Ni kituo kikuu cha kuendesha mnada wa kahawa, zao ambalo ni mhimili muhimu wa kiuchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro. Pamoja na zao hili la kahawa linalolimwa kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro, kilimo cha mpunga na miwa kinaendeshwa kwenye nyanda za chini.
Watalii wengi wanaokuja Moshi zaidi ni wale wanaojiandaa kwa safari ya kupanda Kilimanjaro, mlima ambao umezungukwa na mashamba ya migomba na kahawa, na kilele chake kufunikwa na barafu.Safari nyingi za kupanda Mlima Kilimanjaro huanzia mjini Moshi kuelekea kwenye vituo maalaum vinavyoendeshwa na Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Mji huu wa Moshi unaongoza kwa usafi nchini Tanzania, na maagizo yametolewa na Manispaa kwa kila mkazi kuwa “msimamizi” wa usafi wa mji.



Je ulikuwa wajua?


