Mtwara
Mli wa Mtwara uko kusini mashariki ya kwenye pwani ya Bahari ya Hindi kuelekea mpakani na Msumbiji. Ukiwa kwenye nyanda za juu tambarare za Makonde, mji huu una kumbukumbu muhimu ya Kanisa la Mt. Paulo lenye kuta zilizochorwa matukio ya kibiblia tangu enzi za uongozi wa wamisinari wa Kijerumani.
Ukiwa karibu sana na Hifadhi ya Bahari ya Mnazi Bay na Mkondo wa Mto Ruvuma, Mtwara unawapa waogeleaji na wapiga mbizi fursa ya kuwa kwenye maeneo ambayo hayatembelewi mara kwa mara na watalii.
Mji huu ulijengwa na wakoloni wa Kiingereza kama kituo kikuu cha kuendeshea mradi wa kilimo cha karanga katika pwani kusini. Mradi huu maarufu uliojulikana kama Nachingwea Groundnut Scheme ulitekelezwa baada ya Vita Kuu ya Pili kwa madhumuni ya kufidia upungufu wa chakula nchini Uingereza na pia kama zao la biashara barani Ulaya.
Mtwara kuna uwanja wa kuweza kupokea hata ndege kubwa na bandari yake inaandaliwa kuwa njia nyingine kuu ya kupitisha mizigo kwenda nchi za jirani kusini magharibi mwa Tanzania hasa mradi wa Mtwara Corridor utakapokamilika.



Je ulikuwa wajua?


