; Musoma » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Musoma

Mji wa Musoma uko kando kando mwa Ziwa Victoria karibu na mpaka na Kenya. Umaarufu wa mji huu unatokana na kijiji cha Butiama, alikozaliwa Rais wa kwanza na Baba wa Taifa wa Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere.

Katika kijiji hiki kuna Makumbusho ya Mwalimu Nyerere ambamo kumehifadhiwa nyaraka, zikiwemo kulizaliwa kwa utaifa, kupigania uhuru pamoja na historia ya Tanzania. Nyaraka nyingine ni pamoja na tafsiri kwa Kiswahili za vitabu vya Shakespeare, Plato’s Republic, Vitabu vya Injili pamoja na Matendo ya Mitume na maandishi mengi yake mwenyewe. Butiama sasa ni mahali pa hija kutokana na watu kwenda kutembelea kaburi la Mwalimu Nyerere.

Jambo jingine la kuvutia katika mji wa Musoma ni aina mbalimbali za vyombo vya usafiri wa majini, kuanzia mashua, boti, ngarawa hadi mitumbwi ambavyo matumizi yake yameshamiri sana ziwani.

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?