Mwanza
Maelezo kuhusu vivutio katika Jiji la Mwanza
Jiji la Mwanza ndiyo bandari kuu katika Ziwa Victoria na ni kitovu cha shughuli cha uchumi katika kanda ya Ziwa. Hili Ziwa ndilo linalounganisha nchi jirani za Afrika Mashariki za Uganda kwa upande wa kaskazini-magharibi na Kenya upande wa kaskazini-mashariki. Usafirishaji kati ya nchi hizi ni msingi mkuu wa uchumi wa Jiji la Mwanza.
Ardhi inayolizunguka jiji imetengwa mahsusi kwa ajili kilimo hasa zao la pamba., chai na kahawa. Sehemu kubwa ya mazao yanayolimwa katika ukanda wote wa Ziwa husafirishwa kupitia Jiji la Mwanza. Uwingi wa viwanda katika maeneo ya bandarini pamoja na mitaa iliyochangamka ni burudani tosha katika Jiji la Mwanza
Jiji la Mwanza hutoa fursa kwa watalii kupanga safari zao za kwenda kuona Hifadhi Taifa ya karibu ya Kisiwa cha Rubondo chenye aina nyingi ya ndege na pia kuelekea kwenye sehemu za magharibi za Serengeti. Uzuri wa Mwanza kuwa karibu sana na mbuga ya Serengeti ni mtalii anaweza kutembelea mbuga hii bila kukumbana na bugudha ya misururu ya magari. Karibu na Jiji la Mwanza kuna Jumba la Makumbusho la Bujora ambako watalii wanaweza kuona vitu vingi vya kitamaduni hasa wa kabila la Wasukuma.



Je ulikuwa wajua?


