; Tanga » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Tanga

Mji wa Tanga unayo bandari ambayo ni ya pili kwa ukubwa baada ya Dar es Salaam na ni maarufu kwa usafirishaji nje wa mazao.

Kwenye maeneo ya zamani, kuna majengo ambayo ni ya enzi za utawala wa kikoloni pamoja na nyumba chache zilizojengwa na Waarabu, kitu ambacho kinaupamba mji kihistoria na uthibitisho wa ushiriki wake kwenye biashara iliyoshamiri katika Bahari Hindi.

Awali, Tanga ilikuwa inashindana na Pangani na Bagamoyo kwa kuwa kiungo cha misafara ya biashara ya watumwa na meno ya ndovu ikitokea Afrika ya Kati. Wakoloni wa Kijerumani mwanzoni mwa karne ya 20  waliufanya mji wa Tanga kuwa mojawapo ya makao ya utawala wao.

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?