; TAARIFA KWA VYOMBO KWA HABARI » Tanzania Tourist Board
 
Language English Kiswahili

TAARIFA KWA VYOMBO KWA HABARI

MAONESHO YA KITALII YA WTM YAENDELEA LONDON -UINGEREZA


Maonesho ya Utalii yajulikanayo kama World Travel Market – WTM ambayo hufanyika mjini London, nchini Uingereza kila mwaka, mwaka huu yameanza tarehe 4 na yataendelea hadi tarehe 7 Novemba, 2013. Jumla ya Kampuni 47 kutoka Tanzania zinashiriki maonesho haya katika banda la Tanzania, chini ya uratibu na usimamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania-TTB.

Maonesho haya yanafanyika wakati Tanzania, katika miaka ya hivi karibuni, imetambuliwa na taasisi mbalimbali duniani kwa ubora wa vivutio vyake na kuimarika kwa utalii katika maeneo mbalimbali. Taasisi ya World Economic Forum iliiweka Tanzania katika nafasi ya pili duniani, baada ya Brazil, kwa ubora wa maeneo ya wanyamapori ambayo yana aina nyingi za wanyama. Taasisi za Lonely Planet na New York Times ziliitaja Tanzania kuwa ni nchi nzuri ya kutembelewa na wageni wanaopendelea vivutio vya asili. Aidha Taasisi ya Seven Natural Wonders nayo ilitangaza vivutio vitatu vya Tanzania ambavyo ni Hifadhi ya Serengeti, Hifadhi ya Ngorongoro, na Mlima Kilimanjaro kuwa miongoni mwa maajabu saba ya asili ya Bara la Afrika. Nayo taasisi ya Safari Bookings.com imeiweka Tanzania kama kituo cha Utalii (tourist destination) cha kwanza kwa ubora katika Bara la Afrika.

Utafiti wa hivi karibuni, uliofanywa na taasisi ya CheapOAir,  umeonesha kwamba Tanzania ni nchi ya kwanza ambayo watalii wa kipato cha wastani wameanza kuitembelea kwa wingi, baada ya kupungua kwa nauli za ndege kwa asilimia sita, wakati nauli za kwenda kwa washindani wetu wengine zimepanda. Moja ya sababu za kushuka kwa nauli za ndege ni kutokana na ushindani wa mashirika kadhaa ya ndege ambayo kwa sasa yanatua katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, hususan KLM, Qatar Airways, na Turkish Airlines. Mashirika mengine ni Kenya Airways na Ethiopian Airlines.

Baadhi ya mawakala wa Utalii wameeleza uwezekano wa kuongezeka kwa idadi ya watalii zaidi ya 1,077,058 iliyofikiwa 2012. Wamedokeza kuwa bookings za watalii zimeongezeka kwa 50% zaidi ya zile za 2012. Kutokana na hali hii, inatarajiwa kwamba hadi Desemba 2013, idadi ya watalii itakuwa imeongezeka kwa zaidi ya asilimia ya 20%.

Uingereza ni soko linaloongoza kwa idadi kubwa ya watalii wanaotembelea Tanzania, ambapo mwaka 2012 watalii 70,000 walikuja kutoka Uingereza pekee. Maonesho haya ya WTM ni moja ya njia ya kuitangaza Tanzania katika soko hili ,kwa lengo la  kuongeza idadi ya watalii kutoka Uingereza na sehemu nyingine duniani.

 

Imetolewa na:

Bodi ya utalii Tanzania

Contact Information

Contacting us by post Tanzania Tourist Board
Utalii House - Laibon street/Ali Hassan Mwinyi Road - Opposite French Embassy
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email md@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General: +255 22 2664878/9
Marketing:+255 22 2664875
Tourism Services:+255 22 2664873
  • Branch Offices
  • Contacting us by fax

    Did you know!

    That Freddy Uiso, is the only contestant from Africa to participate in the World Chef Championship Competition and to be nominated for World Chef Title and become the 4th winner?".

    S!TE TO RESUME 2017!