Milima na Volkano
Ingawa Mlima Kilimanjaro fahari ya Afrika na ni mrefu kuliko milima yote katika bara hili, bado Tanzania inajivunia kwa kuwa na safu ya milima mingine yenye vilele vya kuvutia. Milima mingi yenye volkano iko katika kanda ya kaskazini na mashariki ya Tanzania.
Safu hii ya milima hutofautiana kuanzia bonde la kuvutia la Mlima Meru na volcano hai ya Ol Donyo Lengai kuelekea kwenye Milima tulivu ya Usambara na miteremko latifu ya bonde la nyanda za juu.
Safari za kutembea kwa miguu pamoja na kupanda milima nchini Tanzania ni kivutio kikubwa kwa watalii wengi ambao wanaona hatoshi kuangalia wanyama wakiwa kwenye misururu ya magari.



Je ulikuwa wajua?


