Milima ya usambara
Milima ya Usambara ni sehemu ya Milima ya Tao ya Mashariki upande wa kaskazini mashariki mwa nchi. Milima ya magharibi na mashariki imetenganishwa na bonde la upana wa kilometa 4 na ndiko kuna makazi na mashamba pamoja na njia za watalii waenda kwa miguu kuelekea kileleni. Sehemu hii kuna wajasiliamali wengi wanaoendesha biashara ya vipepeo hai.
Njia hizi zinawaelekeza watalii kupitia kwenye maeneo yenye baionuwai ya pekee barani Afrika. Kutoka kileleni kunaonekana mandhari nzuri za Nyika za Masai kwa upande mmoja na upande mwingine inaweza kuonekana Bahari ya Hindi.



Je ulikuwa wajua?


