Mlima meru
Maelezo kuhusu vivutio vya Mlima Meru
Bonde hili la kuvutia katika Mlima Meru, mara nyingi linapunguzwa hadhi yake na umaarufu wa vivutio vilivyoko upande wa mashariki, hata hivyo kuutembelea mlima huu ambao uko kwenye Hifadhi ya Taifa ya Arusha, unampa mtalii burudani ya aina yake. Miteremko yake imefunikwa na misitu minene ambako mbega wanapata mazingira ya kufurahia huku nyati nao wakitulia kivulini.
Volkano zimwe liliacha bonde kubwa lililozungukwa na kuta za majabali yaliyochongoka. Kuna mwinuko wa majivu ambao umetengeneza mfano wa kilele kingine. Kutoka kwenye miteremko ya Mlima Meru unaweza kuona vizuri mandhari ya Maziwa ya Momela na Bonde la Ngurdoto.



Je ulikuwa wajua?


