; Mlima kilimanjaro » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Mlima kilimanjaro

Mlima Kilimanjaro uliofunikwa na theluji kileleni unajichomoza kwenye tambarare za uwanda katika nyanda za juu kaskazini mwa Tanzania ikitiririsha mito ya theluji. Mlima huu ambao uko karibu na mji wa Moshi ni Hifadhi ya Taifa na huangaliwa sana ili mazingira yake yasichafiliwe kwa namana yo yote.

Mifumo ya ekolojia ya mlima huu ni ya aina mbali mbali hivyo huvutia sana. Kwenye miteremko ya chini ya mlima kumeshamiri sana kilimo cha mibuni, migomba na mahindi kwa ajili ya mazao ya biashara na chakula. Pamoja na kuweko na mashamba makubwa machache ya mibuni shughuli za kilimo nje ya Hifadhi, zinaendeshwa na wakulima wadogo wadogo kwenye vihamba.

Mara tu unapoingia kwenye Hifadhi unakumbana na msitu ambao unene wake  unapungua kadiri unavyopanda hadi unafikia makonde ya nyasi yenye hewa pungufu. Kuelekea kileleni maumbile ya mlima huwa na ardhi kame yenye miamba na barafu ambacho ndio kivutio kikuu Barani Afrika.

Kupanda Mlima Kilimanjaro ni kumbukumbu ya pekee kwa watalii wanaokuja Tanzania. Kutoka juu ya Mlima Kilimanjaro unapata mandhari nzuri ya Bonde la Ufa, mbuga za wafugaji wa Kimasai na Mlima Meru. Pia unaweza kuona Hifadhi ya Amboseli ya  Kenya kutoka mlima huu.

Mlima Kilmanjaro wenye urefu wa mita 5896 kutoka usawa wa bahari unaonekana kutoka sehemu nyingi, lakini kuupanda huu mlima ni lazima kuja Tanzania. Kutokana na njia nyingi za kufikia kilele chake, mtu ye yote anaweza kuupanda mlima huu kufutana na msimu na idadi siku atakazochukua.

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?