; Selous » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Selous

Mbuga ya Wanyama ya Selous iko kusini mashariki mwa Tanzania ni kubwa kuliko zote barani Afrika na inachukua zaidi ya 6% ya eneo lote la Tanzania. Mito, vilima na mbuga zake ni makazi murua ya makundi ya tembo wanaorandaranda, wakiwemo faru weusi waliobakia na pia idadi kubwa ya mbwa mwitu.

Kiutalii mbuga hii imegawanywa kwenye sehemu mbili. Sehemu ya kaskazini ndiyo hutembelewa na watalii wengi ikilinganishwa na kusini ambayo imetengwa mahsusi kwa ajili ya shughuli za uwindaji.

Kivutio chake maalum ni Mto Rufiji ambao unapokea maji toka Mto Ruaha kwenye sehemu inayojulikana kama Korongo la Stiggler na hatimaye kuishia katika Bahari Hindi. Kwenye bonde la Rufiji ambalo ni kubwa sana kuliko mengine hapa Tanzania ni makazi mahsusi ya viboko, mamba na ndege wanopenda mazingira ya maji maji.Kufuatana na majira utalii wa kutumia usafiri wa boti umetokea kupendwa zaidi.

Hata hivyo Mbuga ya Selous ni maarufu kwa kuwa na idadi kubwa ya wanyamapori. Inakadiriwa kuwa na 50% ya tembo wote nchini, 25% ya nyati waioko barani Afrika.

 

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?