; Ukanda wa safari » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Ukanda wa safari

Pamoja na kuwa na hifadhi nyingi na ratiba tofauti, Tanzania imegawanywa katika maeneo mbali mbali ya kitalii kufuatana na hali ya nchi. Hata hivyo kuna kanda nyingi zinazotembelewa zaidi ya nyingine, hasa ukanda wa kaskazini. Hali hii inatokana na ukweli kwamba hifadhi nyingine hazijulikani sana kwenye soko.

Ukanda wa Kusini unajumuisha pia Mbuga ya Selous ambayo ni kubwa kuliko mbuga zote barani Afrika na inaizidi hata nchi ya Denmark. Pamoja na umaarufu wa utalii katika ukanda wa kaskazini, lakini inashauriwa wageni watembelee na sehemu nyingine wajionee wenyewe utajiri wa nchi hii.

Inayofuata ni maelezo mafupi kuhusu vivutio muhimu vya utalii katika kila ukanda nchini Tanzania. Ingawa kanda za magharibi na mashariki hazijaen-delezwa kiasi cha kutosha, bado kuna vitu vingi vinavyoweza kuwavutia wageni au wasafiri wanaopenda kujifunza ama kujionea mambo mapya.

Kwa kweli kanda inayojitosheleza. Taarifa zilizotolewa ni kama mwongozo tu kwa mtalii anayekuja kwa mara ya kwanza ama yule aliyewahi kuja lakini anatafuta mahali mbadala pa kutembelea. Hata hivyo makampuni ya kitalii yanaweza kutoa ushauri kuhusu maeneo yanayofaa kutembelewa na wakati gani. Kwa maelezo zaidi kuhusu maeneo haya yanapatikana  kwenye taarifa mahsusi za Hifadhi za Taifa na Mbuga za Wanyama.

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?