Mafia
Maelezo kuhusu Vivutio vya Kisiwa cha Mafia
Mafia ni kisiwa maarufu kwa mapumziko ya watalii baada ya kutembelea vivutio vingine nchini kwa sababu fukwe zake zinatoa fursa ya faragha na starehe. Halikadhalika, Kisiwa hiki huwapa nafasi wapiga mbizi waliobobea kupata burudani ya pekee. Hata hivyo, watalii wengi sasa wanapenda sana kutembelea Mafia.
Kwa karne kadhaa, Kisiwa cha Mafia kilikuwa kituo maalum kwa wafanyabiashara wa Kishirazi. Chini ya utawala wa Sultani wa Oman aliyekuwa na makao makuu Zanzibar, Mafia ilikuwa maarufu sana kwa kilimo cha minazi na mikorosho kilichoendeshwa na wamiliki wa Kiarabu walioishi katika kisiwa kidogo cha Chole. Pamoja na hayo yote, Kisiwa cha Mafia sasa ni Hifadhi ya Bahari ambayo ni kubwa kuliko zote katika Bahari ya Hindi.



Je ulikuwa wajua?


