; Pemba » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Pemba

Maelezo kuhusu vivutio vya Utalii katika Kisiwa cha Pemba

Kisiwa cha Pemba pamoja na Unguja vinaunda Zanzibar ambayo iko katika Bahari ya Hindi, mashariki mwa Tanzania Bara. Kisiwa hiki kiko umbali wa kilometa 46 kaskazini-mashariki mwa Unguja. Pia kina urefu wa kilometa 64 na upana kilometa 22. Visiwa hivi viwili vinatenganishwa na “Mlangobahari wa Pemba” (Pemba Channel).

Mandhari ya Pemba ni ya vilima vilima ambako ni makazi ya watu na mabonde yanayotumika kwa kilimo cha mpunga, viazi na matunda. Karafuu, minazi na pilipili manga hustawi zaidi kwenye miteremko na maeneo tambarare. Kutokana na utajiri huu Waarabu  walikiita kisiwa hiki “Jazora al Khudra” ikimaanisha “Kisiwa cha Kijani”.

Kiutalii “Mlangobahari wa Pemba”  ni njia maarufu ya nyangumi. Kufuatana na nyaraka za Shirika la Utalii Duniani (WTO), Pemba ina asilimia 25 ya maeneo ya kupiga mbizi yenye hadhi ya kimataifa ulimwenguni.  Pia kuna visiwa vidogo vidogo vyenye vivutio vya kipekee vya kitalii, mfano mzuri ni Kisiwa cha Misali ambacho sasa ni hifadhi. Kivutio kingine ni Hifadhi ya Msitu wa Ngezi.

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?