; Historia ya Tanzania » Tanzania Tourist Board
 
Badilisha Lugha English Kiswahili

Historia ya Tanzania

Historia ya Tanzania

Tanzania – Usuli (Brief history)

Mara baada ya uhuru kutoka kwa Mwingereza kwenye miaka ya 1960 Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda taifa la Tanzania mwaka 1964.

Ikiwa  si mbali sana kusini  mwa mstari wa Ikweta, Tanzania ambayo sasa ina idadi ya watu 42,000,000 ni nchi kubwa kuliko zote Afrika Mashariki yenye vivutio vingi vya kitalii. Tanzania imejaliwa vivutio vingi vya kiwango cha kimataifa, kama Mlima wa ajabu wa Kilimanjaro wenye barafu kileleni karibu na Ikweta na ni mlima mrefu kuliko yote barani Afrika. Pia kuna Serengeti, Ngorongoro na visiwa za Zanzibar vilivyopambwa na mikarafuu na minazi inayopeperusha upepo murua ufukweni mwa Bahari ya Hindi, bila kusahau mandhari ya Mji Mkongwe…Tukiacha maajabu yaliyoainishwa hapo juu Tanzania ina mambo mengine mengi ya kuvutia.

Kokote utakakokwenda nchini Tanzania utakuta mandhari nzuri na utawaona aina mbali mbali ya wanyamapori waliotulia na kupendeza ukiwaangalia. Karibu asilimia 30% ya nchi imehifadhiwa kisheria kwa ajili ya wanyamapori. Kwa mfano katika mbuga za savana wanapatikana wanyamapori wa aina mbali mbali wakiwemo wale maarufu – tembo, simba, faru, nyati na chui.

Tanzania imebahatika kuwa moja kati ya maeneo manne duniani maarufu kwa bioanuwai. Ni moja kati ya nchi chache barani Afrika zinazoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya aina mbali mbali ya mamalia. ndege na vipepeo. Licha ya hayo  Tanzania kuna tamaduni tofauti za kuvutia, burudani na michezo ya kuogelea na kupiga mbizi katika maji tulivu ya bahari. Kweli ukifika Tanzania utapata mapumziko na starehe, kitu ambacho hutosahau maishani. Kiuchumi, bandari yake ya Dar es Salaam ni kiungo muhimu kati ya nchi nane za Afrika ya Kati na Kusini na nchi nyingine nje ya Bara la Afrika.

Pamoja na vivutio mbali mbali vya asili, Tanzania, nchi yenye makabila zaidi ya 120, inasifika kwa kuwa na watu wakarimu wasio na majivuno, lakini wenye msimamo. Mgeni popote anapokwenda anapokelewa kwa heshima, upendo na urafiki wa dhati.

Mawasiliano

Contacting us by post Bodi ya Utalii
Jengo la IPS,Gorofa ya tatu
P.O.Box 2485
Dar-es-Salaam
Tanzania.
Contacting us by email info@tanzaniatourism.go.tz
Contacting us by telephone
General (+255) 022 2111244/5
Mkurugenzi Mwendeshaji 2110908
Masoko 2111345
Huduma za Kitalii 2128472
Utafiti 2111514
Contacting us by fax (255) 022 2116420

Je ulikuwa wajua?

Kuwa Dar-es-salaam ilikuwa ni kijiji cha uvuvi kilichojulikana kama ‘Mzizima’?